SOMO: BADO KUNA HATUA KATIKA KUMJUA MUNGU
MHUDUMU: SAMWEL JOSEPH KAZIMILI
Nini maana ya Kumjua Mungu?
Ø Ni ile hali ya kuuelewa ukuu wa Mungu kwa mapana zaidi na kuendelea kujifunza kanuni na sheria za Mungu ili tuweze kutembea ndani ya kusudi la wito/ uumbaji wake.
AYUBU 22:21-22, YEREMIA 24:7, ZABURI 19:7-8, YOSHUA 1:7-8.
Ø Kumjua Mungu ni kitendo au zoezi endelevu kwa maana hiyo hakuna hatua ambayo mtu/mwanadamu atasema amefika mwisho katika kumjua Mungu.
Mfano: KUTOKA 6:2-3. Ibrahimu Baba yetu wa imani aliujua ukuu wa Mungu lakini bado kuna vitu vya kimungu havikufunuliwa kwake.
Katika kumjua Mungu mambo yafuatayo ni muhimu:
a) Shauku/kutamani/kuadhimia kutoka ndani. ZABURI 1:1-3, 27:4, 122:1
b) Kufanya/kutenda ili kuitimiza shauku yako.
ZIFUATAZO NI BAADHI YA NJIA ENDELEVU KATIKA KUMJUA MUNGU.
1) Maombi. LUKA 18: 1-7.
2) Kusoma neno na kuliishia neno. ISAYA 66:2.
3) Ushirika na Mungu(Ibada). KUMB. 6:5, 12:11-13.
4) Huduma.
5) Utoaji.
6) Uaminifu.
7) Shukrani.
8) Sifa.
9) Kujazwa Roho Mtakatifu. 1KORINTHO 2:10-12.
FAIDA ZIPATIKANAZO KATIKA KUMJUA MUNGU.
ü Muonekano wako wa nje na ndani utafanywa upya:
· Tabia (Tabia za maroho zitaondolewa na tabia za Roho wa Mungu zitajengeka)
1 TIMOTHEO 4:12, 1 PETRO 1:14-15, EFESO 5: 9.
· Mazungumzo/mawasiliano na watu. ZABURI 37:30.
· Ufahamu katika kufanya maamuzi na katika mambo mbalimbali. KUTOKA 31:1-4,
EFESO 4:29.
· Uvaaji.
· Ujasiri. ZABURI 34: 19-20.
· Imani na madhabahu safi mbele za Mungu. 1 KORINTHO 3: 16-17.
ü Utakuwa na shauku ya kuitambua sauti ya Mungu, Mwanadamu na shetani katika mambo mbalimbali. WAAMUZI 6:17-18, 6:36-40, 13:3-9.
ü Utakuwa ni mwenye subira katika mambo yenye kuhitaji uvumilivu. 27: 14.
ü Matendo yako yatakuwa ni yenye kumpendeza Mungu. KUMB. 28: 9.
ü Nguvu na mkono wa Mungu utakuwa na wewe, kazi za mikono yako, uhai na vizazi vyako. KUMB. 7:12-15, ISAYA 66:22.
ü Utajua namna ya kuingia na kutoka mbele za Mungu. HESABU 14:11-20.
No comments:
Post a Comment