Monday, March 16, 2015

SOMO: BADO KUNA HATUA KATIKA KUMJUA MUNGU

MHUDUMU: SAMWEL JOSEPH KAZIMILI
                                       

Nini maana ya Kumjua Mungu?
Ø  Ni ile hali ya kuuelewa ukuu wa Mungu kwa mapana zaidi na kuendelea kujifunza kanuni na sheria za Mungu ili tuweze kutembea ndani ya kusudi la wito/ uumbaji wake.
AYUBU 22:21-22, YEREMIA 24:7, ZABURI 19:7-8, YOSHUA 1:7-8.
Ø  Kumjua Mungu ni kitendo au zoezi endelevu kwa maana hiyo hakuna hatua ambayo mtu/mwanadamu atasema amefika mwisho katika kumjua Mungu.
Mfano: KUTOKA 6:2-3. Ibrahimu Baba yetu wa imani aliujua ukuu wa Mungu lakini bado kuna vitu vya kimungu havikufunuliwa kwake.
Katika kumjua Mungu mambo yafuatayo ni muhimu:
a)      Shauku/kutamani/kuadhimia kutoka ndani. ZABURI 1:1-3, 27:4, 122:1
b)      Kufanya/kutenda ili kuitimiza shauku yako.
ZIFUATAZO NI BAADHI YA NJIA ENDELEVU KATIKA KUMJUA MUNGU.
1)      Maombi. LUKA 18: 1-7.
2)      Kusoma neno na kuliishia neno. ISAYA 66:2.
3)      Ushirika na Mungu(Ibada). KUMB. 6:5, 12:11-13.
4)      Huduma.
5)      Utoaji.
6)      Uaminifu.
7)      Shukrani.
8)      Sifa.
9)      Kujazwa Roho Mtakatifu. 1KORINTHO 2:10-12.
FAIDA ZIPATIKANAZO KATIKA KUMJUA MUNGU.
ü  Muonekano wako wa nje na ndani utafanywa upya:
·         Tabia (Tabia za maroho zitaondolewa na tabia za Roho wa Mungu zitajengeka)
1 TIMOTHEO 4:12, 1 PETRO 1:14-15, EFESO 5: 9.
·         Mazungumzo/mawasiliano na watu. ZABURI 37:30.
·         Ufahamu katika kufanya maamuzi na katika mambo mbalimbali. KUTOKA 31:1-4,
EFESO 4:29.
·         Uvaaji.
·         Ujasiri. ZABURI 34: 19-20.
·         Imani na madhabahu safi mbele za Mungu. 1 KORINTHO 3: 16-17.
ü  Utakuwa na shauku ya kuitambua sauti ya Mungu, Mwanadamu na shetani katika mambo mbalimbali. WAAMUZI 6:17-18, 6:36-40, 13:3-9.
ü  Utakuwa ni mwenye subira katika mambo yenye kuhitaji uvumilivu. 27: 14.
ü  Matendo yako yatakuwa ni yenye kumpendeza Mungu. KUMB. 28: 9.
ü   Nguvu na mkono wa Mungu utakuwa na wewe, kazi za mikono yako, uhai na vizazi vyako. KUMB. 7:12-15, ISAYA 66:22.
ü  Utajua namna ya kuingia na kutoka mbele za Mungu. HESABU 14:11-20.




No comments:

Post a Comment