Tuesday, March 31, 2015

IBADA YA FUNGUA SEMISTER ILIYOFANYIKA TAR.21/3/2015

MATUKIO KATIKA PICHA YA IBADA YA OPEN SEMISTER ILIYOFANYIKA TAG-MCC

praise and worship team wakimwabudu MUNGU
wana-casfeta waliofika katika ibada hiyo waki MWAZIMISHA  MUNGU



Ev. Lameck akihudumu kupitia neno la BWANA

Baadhi ya umati wa wana casfeta wakifatilia neno la MUNGU kwa karibu

 kaka Allan akiongoza ibada

Ev. na Mwalimu Michael akihudumu kwa neno la BWANA 


Uwepo wa BWANA ulikuwepo kuhudumia watu wake




EV. Amandus Sebastian akisema neno katika ibada hiyo

Monday, March 16, 2015

SOMO: BADO KUNA HATUA KATIKA KUMJUA MUNGU

MHUDUMU: SAMWEL JOSEPH KAZIMILI
                                       

Nini maana ya Kumjua Mungu?
Ø  Ni ile hali ya kuuelewa ukuu wa Mungu kwa mapana zaidi na kuendelea kujifunza kanuni na sheria za Mungu ili tuweze kutembea ndani ya kusudi la wito/ uumbaji wake.
AYUBU 22:21-22, YEREMIA 24:7, ZABURI 19:7-8, YOSHUA 1:7-8.
Ø  Kumjua Mungu ni kitendo au zoezi endelevu kwa maana hiyo hakuna hatua ambayo mtu/mwanadamu atasema amefika mwisho katika kumjua Mungu.
Mfano: KUTOKA 6:2-3. Ibrahimu Baba yetu wa imani aliujua ukuu wa Mungu lakini bado kuna vitu vya kimungu havikufunuliwa kwake.
Katika kumjua Mungu mambo yafuatayo ni muhimu:
a)      Shauku/kutamani/kuadhimia kutoka ndani. ZABURI 1:1-3, 27:4, 122:1
b)      Kufanya/kutenda ili kuitimiza shauku yako.
ZIFUATAZO NI BAADHI YA NJIA ENDELEVU KATIKA KUMJUA MUNGU.
1)      Maombi. LUKA 18: 1-7.
2)      Kusoma neno na kuliishia neno. ISAYA 66:2.
3)      Ushirika na Mungu(Ibada). KUMB. 6:5, 12:11-13.
4)      Huduma.
5)      Utoaji.
6)      Uaminifu.
7)      Shukrani.
8)      Sifa.
9)      Kujazwa Roho Mtakatifu. 1KORINTHO 2:10-12.
FAIDA ZIPATIKANAZO KATIKA KUMJUA MUNGU.
ü  Muonekano wako wa nje na ndani utafanywa upya:
·         Tabia (Tabia za maroho zitaondolewa na tabia za Roho wa Mungu zitajengeka)
1 TIMOTHEO 4:12, 1 PETRO 1:14-15, EFESO 5: 9.
·         Mazungumzo/mawasiliano na watu. ZABURI 37:30.
·         Ufahamu katika kufanya maamuzi na katika mambo mbalimbali. KUTOKA 31:1-4,
EFESO 4:29.
·         Uvaaji.
·         Ujasiri. ZABURI 34: 19-20.
·         Imani na madhabahu safi mbele za Mungu. 1 KORINTHO 3: 16-17.
ü  Utakuwa na shauku ya kuitambua sauti ya Mungu, Mwanadamu na shetani katika mambo mbalimbali. WAAMUZI 6:17-18, 6:36-40, 13:3-9.
ü  Utakuwa ni mwenye subira katika mambo yenye kuhitaji uvumilivu. 27: 14.
ü  Matendo yako yatakuwa ni yenye kumpendeza Mungu. KUMB. 28: 9.
ü   Nguvu na mkono wa Mungu utakuwa na wewe, kazi za mikono yako, uhai na vizazi vyako. KUMB. 7:12-15, ISAYA 66:22.
ü  Utajua namna ya kuingia na kutoka mbele za Mungu. HESABU 14:11-20.




Tuesday, March 3, 2015

DAY.2-OUTREACH-MISSION AT MAKUYUNI, KOROGWE-TANGA

KIPINDI CHA KUMSIFU MUNGU NA KUMTUKUZA KATIKA SIKU YA PILI YA MKUTANO






Wainjilisti LILIAN Kulia na BEATRICE kushoto, wakimsindikiza, muinjilisti wa siku ya pili, Ev. GROLY UHAGILE katikati


                                 Ev. GROLY UHAGILE akihudumu
                                Ev. Groly Uhagile akiachilia Gombo katika viwanja vya makuyuni-korogwe TANGA



 watu walimkiri Yesu Kristo, kuwa BWANA NA MWOKOZI WAO, SIKU YA 2 ya mkutano


 watu wakihudumiwa na wahudumu wanafunzi kutoka CASFETA-TAYOMI mzumbe chuo kikuu makuyuni soko la zamani, wilayani Korogwe-Tanga, february 2015