Siku ya Jumamosi ya tarehe 12 Novemba 2016, Familia ya Casfeta Tayomi Chuo Kikuu Mzumbe tuliwakaribisha wapendwa wetu wa mwaka wa kwanza.
Hawa ni baadhi ya mwaka wa kwanza wengi mno ambao wameungana nasi katika Familia yetu ya Casfeta Tayomi Chuo Kikuu Mzumbe.
Ilikuwa ni ibada nzuri sana iliyojaa uwepo na udhihirisho wa nguvu za Mungu
Dr Titus Tossy kama "MENTOR" wetu, aliwakaribisha mwaka wa kwanza na kuwahimiza sana juu ya umuhimu ya kujiandaa kiroho(SPIRITUALLY) na kimwili(ACADEMICALLY) katika mazingira mapya waliyopo na hatua waliyoifikia.
Mwaka wa kwaza wakiwa makini kabisa kusikiliza masomo wanayopewa na Watumishi wa Mungu
Baba yetu mlezi Mchungaji Emmanuel Meshy alikuwa pamoja nasi na alitupatia Neno la Mungu lililobadilisha kabisa fikira zetu ili ziweze kuendana sawasawa na Neno la Mungu
Ibada ilifuatiwa na kulishwa keki kwa mwaka wa kwanza pamoja na wanacasfeta tayomi wenyeji ndani ya Chuo kikuu Mzumbe
Mwenyekiti wa Casfeta Tayomi Chuo Kikuu Mzumbe, Ndg Michael George Kishiwa akiwa makini kabisa kukata keki kwa ustadi ili watu waweze kula
MC wa sherehe hii Ndg David Kunonga Mezza akiwa makini kabisa kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa na Mungu akitukuzwa kwa kila jambo
Tunamshukuru Mungu sana kwa kutusaidia kufanikisha sherehe hii ya kuwakaribisha ndugu zetu mwaka wa kwanza. Na Sifa na Utukufu wote zimrudie yeye maana pekee ndiye anastahili. Amen